Nyota
wa nyimbo za Injili Bongo, Bahati Lusako Bukuku ameumia mgongo na
maeneo kadhaa ya mwili (nusu kifo) kiasi cha kushindwa kukaa, kusimama
wala kutembea kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea kwenye eneo la
Ranchi ya Narco wilayani Kongwa, Dodoma saa tisa usiku wa kuamkia
Jumamosi.
Katika ajali hiyo ambayo Bahati alikuwa akienda Kahama, Shinyanga kwenye mkutano wa Injili, dereva wa gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT 7945, Edison Mwakabungu ‘Eddy’ (31) aliumia sana kwenye vidole vya miguu na hawezi kutembea.
Wengine waliokuwemo kwenye ajali hiyo ni wacheza shoo wa Bahati, Frank Muha (20) na mwenzake ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Alfajiri ya juzi, mwandishi wa habari hizi alimpigia simu Bahati na kuongea naye kuhusu ajali hiyo ambapo huku akisikika kama anayepata tabu kwa maumivu, alisema:
“Ni kweli tumepata ajali, nimeumia mgongoni, dereva ameumia mguu. Namshukuru Mungu. Sijui nini kilitokea, nilishtukia kuona gari kubwa mbele yetu likituvaa, mara nikashtukia tuko porini. Lakini kabla ya safari Dar tulifanya maombi makubwa, najua Mungu ametunusuru na kifo kibaya,” alisema Bahati

0 Komentar untuk "BAHATI BUKUKU ANENA MAZITO BAADA YA KUKWEPA KIFO"