Ni
kitu ambacho hakuna mtu ambaye aliwahi kuhisi au kutegemea kama
Marehemu Adam Kuambiana ambaye alikua muongozaji[Director] wa filamu
nyingi za Kitanzania kumbe nae kashiriki kwenye video ya Mdogo
Mdogo.Adam Kuambiana ambaye alifariki May 17 2014 wakati akiwa kambini
kwa ajili ya filamu yake mpya ametajwa na Diamond kuhusika na
utengenezaji wa Script[muongozo] wa video ya Mdogo Mdogo iliyotengenezwa
South Africa na God Father.
Diamond
ameongea na XXL na kusema>>’Script wakati inaanza nilikua kama
natamani nifanye kitu fulani lakini nilikua sijui naanzaje sasa
nakumbuka kipindi hicho Adam Kuambiana walikuwa wana shoot na kuongoza
movie ya wakina baby[Wema] mimi nilipokua naenda kambini nakutana naye’
‘Baby
alinambia ni mzuri sana nikamfata nikamwambia nina nyimbo yangu nataka
uniandikie stori wimbo wangu unaenda hivi na hivi akanambia ni vizuri
nikifika studio niisikilize kwanza huo wimbo’
‘Nikawa
nae studio nakumbuka nilikuwa nae studio kwa Tudd Thomas pale THT akawa
anasikiliza wimbo akawa ananambia namna stori inavyotakiwa kwenda so
naweza kusema stori inavyoanza picha hata ya kupata Stori ni Kuambiana
ndiye aliyenipa.
Tag :
Cate-Udaku
0 Komentar untuk "DIAMOND AFAFANUA KUHUSU MAREHEMU KUTOKEA KWENYE VIDEO YAKE"