Mwili wa kijana Paschal Jumbe ukiwa kitandani baada ya kujiua
Kijana
mmoja aliyejulikana kwa jina la Paschal Jumbe (35) mkazi wa mtaa wa
Mission katika kata ya Kalangalala wilaya ya Geita mkoani Geita amekutwa
amekufa katika nyumba anayoishi kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni msongo wa mawazo.
Akizungumzia
tukio hilo mwenyekiti wa mtaa huo Juma Kajala amesema kuwa tukio hilo
limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo saa 2.30 asubuhi alipigiwa simu
na watu wanaoishi naye kwenye nyumba hiyo.
Amesema
baada ya kufika hapo alikuta dirisha likiwa limefunguliwa na marehemu
akiwa amelala kitandani ndipo alipiga simu polisi na walipofika polisi
walivunja mlango na kumkuta akiwa amekufa.
Naye dada wa marehemu Nyanyama Jumbe alisema kuwa mdogo wake alikuwa na ugonvi wa
kifamilia na mke wake Reticia Jumbe ambaye walipogombana alikwenda
kuishi eneo la Nyankumbu nje kidogo ya mji na huenda ndicho chanzo cha
mdogo wake kujinyonga.
Kamanda
wa polisi mkoani hapa Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio na
kwamba uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo unaendelea.
Tag :
MAJANGA
0 Komentar untuk "JAMAA AKUTWA AMEJIUA KITANDANI KWAKE....click ujue sababu"