MAJANGA: MKE WA KINGWENDU ABAKWA
MKE wa Kingwendu ambaye ni muigizaji maarufu wa filamu za vichekesho nchini amefanyiwa
kitendo kibaya cha ubakaji na mwanaume aliyefahamika kama
Upunguvuku katika pagala moja huko Mbagala Kingugi kwa Kisauti.
Mke
wa Kingwendu anayejulikana zaidi kwa jina la mama Maua,
alikutwa na masahibu hayo Alhamisi iliyopita baada ya kuvamiwa
na Upunguvuku anayedaiwa kuwa alikuwa amelewa na kuingizwa
kwenye jumba ambalo halijakamilika kujengwa lililopo maeneo ya
Kwa Dunga ambapo wapita njia waliwafuma na kuanzisha
mtiti....
Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina
lake liandikwe amesema kuwa, wakati tukio hilo linatokea,
Kingwendu mwenyewe alikuwa safarini na hivyo majirani zake ndio
waliomuokoa mkewe......Hata hivyo baadhi ya majirani
walioongea na mwandishi wamedai kuwa wawili hao ( Upunguvuku na
mama Maua) ni wapenzi wa siku nyingi na wamekuwa wakionekana
mara kadhaa wakienda kunywa pombe za kienyeji.....
"Huyu
Upunguvuku ni fundi Mwashi, tunamfahamu vizuri kuwa ni hawara
wa mama Maua, mara kadhaa huwa tunawaona wakinywa pombe za
kienyeji pamoja, sema tu leo wamefumwa wakijivinjari ndo
mwanamke anamsingizia eti kambaka," alisema shuhuda mmoja.
Juhudi
za kumpata Kingwendu kuongelea mkasa huo hazikuzaaa matunda
kutokana na simu yake kutopatikana kila akipigiwa..
-Kwa Taarifa zaidi juu ya TUKIO hili tutawajulisha hapa hapa pindi uchunguzi utakapokamilika.
0 Komentar untuk "MAJANGA: MKE WA KINGWENDU ABAKWA"