Mahaba matamu: Wawili hao walikula raja sana mjini Miami
BAADA
ya matokeo mabaya katika Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya taifa,
Italia, mshambuliaji Mario Balotelli amepigwa picha akivuta sigara na
kufanya matanuzi na mpenzi wake Fanny Neguesha mjini Miami, Marekani.
Mshambuliaji
huyo wa Milan, ambaye alipigwa faini na klabu yake kwa kuvuta sigara
kwenye treni mwaka jana, haonekani kabisa kuwa na dalili za kuacha
sigara baada ya kupigwa picha akiwa kwenye korido la hoteli anavuta.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 23 yupo mapumzikoni na mpenzi wake, Fanny
Neguesha baada ya Kombe la Dunia ambako alifunga bao moja tu dhidi ya
England, Italia ikitolewa hatua ya makundi.
Kitu laini: Balotelli akivuta sigara kwa hisia kali mjini Miami
Niinue baba: Balotelli akiwa amembeba mpenzi wake baharini
Akiwa
mapumzikoni, Balotelli pia aliposti picha akiwa na mkanda wa ubingwa wa
dunia wa UFC World katika akaunti yake ya Instagram.
Mtaliano huyo awali alisema kwamba kama asingekuwa mwanasoka, angeibukia kwenye mchezo wa sanaa za mapigano.
Balotelli anafikiriwa yuko njiani kuondoka Milan, ambako alitua miezi 18 iliyopita akitokea Manchester City.
Balotelli akiwa na mkanda wa ubingwa wa UFC
Balotelli akiwa na mashabiki wake katika ufukwe mjini in Florida
Milan
iko tayari kumuuza mshambuliaji huyo ili kupunguza bajeti yao ya
mishahara, huku Arsenal ikiwa miongoni mwa klabu zinazomtaka.
Balotelli
anataka kurudi Ligi Kuu ya England, lakini kocha wa Arsenal, Arsene
Wenger amekanusha kuwa na mpango wa kumsaini mshambuliaji huyo.
0 Komentar untuk "MARIO BALOTELI AONDOA NUKSI ZA KOMBE LA DUNIA NA MAMITO, click kwa picha zaidi"