Nyota mpya wa Arsenal, Alexis Sanchez akiwa ndani ya 'uzi' mpya.
MSHAMBULIAJI mahiri wa Chile na
Barcelona, Alexis Sanchez, amejiunga na Klabu ya Arsenal kwa pauni
milioni 30 na mkataba wa miaka miaka minne.
Akiwa klabuni hapo, nyota huyo atalipwa
pauni 140,000 kwa wiki sawa na Mesut Ozil aliyekuwa analipwa kiasi hicho
kikubwa kuliko wote ndani ya timu hiyo ya London.
Sanchez amekatiza likizo yake
kukamilisha uhamisho huo na kufanyiwa vipimo ambapo mkataba wake huo una
kipengele cha uwezekano wa kuongeza miezi 12 zaidi.
Kwa kujiunga na mabingwa hao wa Kombe la
FA, Sanchez amemwandalia mazingira mazuri mshambuliaji wa Liverpool na
Uruguay, Luis Suarez kutua Barcelona kuziba pengo lake kwa uhamisho wa
pauni milioni 75.
Tag :
cate-michezo
0 Komentar untuk "SANCHEZ ATUA RASMI ARSENAL...mcheki kwenye uzi wa arsenal"