Flickr Photos

Gallery

USAJILI ULIOFANYIKA NA UNAONGOJEWA KWA HAMU LIGI KUU


Arsenal watakamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka Chile, Alexis Sanchez, 25 anayechezea Barcelona siku ya Jumatano, kwa mujibu wa Arsene Wenger (Talksport), Tottenham wametoa dau jipya na 'kuuteka' mchakato wa Liverpool wa kumsajili kiungo wa Lille Divock Origi (Daily Mirror),
Juventus wamewasilisha tena dau la pauni milioni 2 kumsajili beki wa Manchester United Patrice Evra, 33 (daily Mail), Iwapo Evra atakwenda Turin, kiungo kutoka Chile, Arturo Vidal, 27, huenda akaweza kwenda Old Trafford kwa kitita cha pauni milioni 32 (Daily Express),
mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Eduardo, 31, amewaaga wachezaji wenzake wa Shaktar Donetsk huku kukiwa na taarifa kuwa atajiunga na Flamengo ya Brazil (Sky Sports),
Roma na Napoli za Italia pamoja na mabingwa wa Ubelgiji Anderlecht wamepanda dau kumsajili beki wa kulia wa Marekani DeAndre Yedlin, 21, ambaye aliichezea Seattle Sounders ya Marekani msimu uliopita (Sky Sports),
Paris St-Germain wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kumnunua kiungo mfaransa Paul Pogba, 21, kutoka Juventus (Le Figaro), Juventus pia wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 21 (Marca) mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba, 36, anasuburi huenda Juventus wakamuita baada ya kumaliza mkataba wake na Galatasaray ya Uturuki (Tuttosport),
Arsenal wanakaribia kupata saini ya Loic Remy kutoka QPR. Timu hizo mbili karibu zinakamilisha makubaliano juu ya ada ya uhamisho, ingawa Remy bado hajazungumzia maslahi binafsi na Gunners (Daily Mirror),
baada ya kukamilisha mikataba ya Alexis Sanchez na Mathiew Debuchy, mchezaji mwingine anayesakwa na Arsenal ni kiungo wa Real Madrid Sami Khedira. Los Bloncos watamruhusu Khedira kuondoka baada ya kufanikisha uhamisho wa Toni Kroos (Daily Express),
Manchester United wanajiandaa kumnyatia Ricardo Rodriguez anayechezea Wolfsburg, kuziba nafasi ya Patrice Evra (Magazeti mbalimbali),
Atletico Madrid wamekubaliana na Bayern Munich juu ya Mario Mandzukic kwa kitita cha euro milioni 22 (Bild), Everton wanataka kumsajili kwa mkopo Demba Ba kutoka Chelsea (Daily Star),
Niklas Bendtner anatarajiwa kusaini katika timu mpya wiki hii baada ya kuruhusiwa kuondoka na Arsenal (BBC) na winga wa Manchester United, Adnad Januzaj, 19, amepata vitisho kufuatia uamuzi wake wa kuichezea Ubelgiji badala ya Albania au Kosovo, kwa mujibu wa taarifa kutoka Serbia (Daily Mail).
Tag : SOCCER, SPORTS
0 Komentar untuk "USAJILI ULIOFANYIKA NA UNAONGOJEWA KWA HAMU LIGI KUU"

Back To Top