Msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma
amefunguka mbele ya paparazi kuwa tangu mume wake Juma Kilowoko ‘Sajuki’
afariki dunia, wamekuwa wakijitokeza wanaume kibao wakitaka kumuoa
lakini amegundua wengi wana nia ya kunitumia tu.
Akizungumza na paparazi hivi karibuni,
Wastara alisema kama mwanamke amekuwa akitamani kumpata mwanaume wa
kumfariji lakini kinachomchanganya ni sampuli ya wanaume wanaotuma
maombi kwake.
“Mpaka sasa wameshanitokea wanaume zaidi
ya kumi lakini wengi wao nawaona wananitaka ili kujua nini nilichonacho
na wengine wananifuata wakidhani watapata mali na si mapenzi ya dhati.
“Kimsingi wanataka tu kujua Sajuki
alidata na nini kwangu, mimi siko hivyo. Siwezi kumruhusu mtu aingie
kwenye maisha yangu kwa masilahi yake. Ninayemhitaji namjua moyoni na
ipo siku nitampata kwani siangalii mfuko wa mtu, naangalia tabia,”
alisema Wastara.
Tag :
Cate-Mapenzi,
Cate-Udaku
0 Komentar untuk "WASTARA "WANANITONGOZA ILI WANICHEZEE ALAFU......""