Rais Uhuru
Kenyatta wa Kenya ni miongoni mwa Marais wachache wenye umri mdogo
kulinganisha na Marais wengi ambapo amekua akienda sawa na baadhi ya
mahitaji au tabia ya vijana wengi ikiwemo kujumuika na Wasanii wakubwa
hata wa Kenya kama Jaguar ambae huwa mara nyingi anakuwepo kwenye hafla
za Ikulu..
Hizi
picha zake za Marekani kwa mujibu wa ripota wa Kenya Julius Kepkoich, ni
kwamba mmoja wa Waandaaji wa mkutano wa Brook Business uliowakutanisha
pamoja marais wa afrika na wakuu wa kampuni za kimataifa ni mwimbaji
Akon.
Akon
mwenye asili ya Senegal aliezaliwa miaka 41 iliyopita ni miongoni mwa
wakali wachache kutoka Afrika ambao waliweza kupenda na kuingia kwenye
chati za muziki wa dunia.
Pamoja na
umaarufu na utajiri wake alioupata akiwa anaishi mpaka sasa nchini
Marekani, Akon bado ameendelea kuikumbuka Afrika na hata kwenye baadhi
ya interview zake na anachoandika kwenye mitandao ya kijamii,
anasisitiza watu kuwekeza Afrika.
0 Komentar untuk "UKWELI KUHUSU UHURU KENYATTA KUOMBA NAMBA ZA SIMU ZA AKON"