Flickr Photos

Gallery

ETO'O ASHTAKIWA KWA KUUZA PICHA ZA NGONO NA KUUZA MALAYA


Eto’o anaweza kuuhesabu 2014 kama mwaka mbaya kwake baada ya timu yake ya taifa kufanya vibaya kwenye michuano ya kombe la dunia lakini pia hana Club ya kuichezea baada ya kumaliza mkataba wake na Chelsea, kama hiyo haitoshi kwa sasa kilichombele yake ni kesi nzito Mahakamani.
Kesi hizo za udhalilishaji ni kutokana na kusambaza picha za utupu, vitisho, ununuzi/uuzaji wa binadamu na udanganyifu zimefunguliwa kwenye Mahakama moja jijini Yaounde, Cameroon ambapo aliezifungua ni aliyekuwa mchumba wake wa zamani Hélène Nathalie Koah.
Mapema wiki iliyopita Koah alifungua kesi hizo dhidi ya Eto’o ambaye amekana mashtaka hayo huku hili likiwa limetokea siku chache baada ya kusambaa kwa picha zake za utupu kwenye mtandao Facebook ambazo mhudumu huyo wa zamani wa ndege amesema zimesambazwa na Eto’o aliyekuwa mpenzi wake.
Eto’o amekanusha kuhusika na hilo na katika kujibu mapigo mchezaji huyo anayeongoza kwa kutwaa tuzo nyingi za uchezaji bora barani Afrika, amefungua kesi ya matumizi mabaya ya fedha($410,755) alizompa Ms Koah kwa ajili ya kufungua taasisi ya kusaidia jamii wakati walipokuwa wapenzi.
Wakati hayo yakiendelea, kaa ukifahamu kwamba Mwanamke huyu alishawahi kuwaingiza kwenye ugomvi mwanamuziki Fally Ipupa na Eto’o baada ya kuwachanganya kimapenzi.
Tag : SOCCER, SPORTS, UDAKU
0 Komentar untuk "ETO'O ASHTAKIWA KWA KUUZA PICHA ZA NGONO NA KUUZA MALAYA"

Back To Top