Flickr Photos

Gallery

HUYU DOGO NI TAPELI BALAA...soma aliyoyafanya



Kevin Fredy Kagengere

Anaitwa Kevin Fredy Kagengere. Ni kijana mdogo lakini tapeli mkubwa sana. Ameshiriki vitendo vingi vya kitapeli hasa kwa wahitimu wa vyuo wanaotafuta ajira.

Amekuwa akidanganya watu kwa kusema anafanya kazi ofisi kubwa kubwa na kuahidi kuwapatia kazi kwa kuwaungamisha na boss wake, kisha anadai hela halafu anatokomea kusikojulikana.

Kisa cha hivi karibuni amemtapeli kijana mmoja (mbaya zaidi wamesoma wote O-level). Alimdanganya yeye ni Procurement officer wa shirika moja kubwa huko Arusha. Na akamwambia kuna vacancy ofisini kwao.
Hivyo akamchomoa jamaa kiasi fulani cha hela. Mbaya zaidi akamfanya jamaa asafiri from Dar to Arusha kwenda kufuatilia kazi hewa. Huu ni uhuni usiovumilika.

Umekula hela ya mtu... basi tulia... badala yake unamdanganya njoo kazini,.. mtu anafunga safari kuja Arusha unampokea kisha unamtelekeza kituo cha mabasi... halafu unazima simu na kutokomea kusikojulikana.

Hebu tafakari ingekuwa wewe ungejisikiaje. Umemaliza chuo, umetafuta kazi bila mafanikio hadi sasa. Anaibuka mtu kukuambia ofisini kwao kuna kazi. Tena mtu huyo ni rafiki yako uliyesoma nae O-Level.
Anakuambia umpe hela ili akupigie kifua upate kazi...unampa... anakuambia njoo Arusha uonane na boss... unafika Arusha anakutelekeza bus terminal..

Hajali kama nauli ukikopa.. hajali kama huna ndugu Arusha... hajali kama utalala nje... hajali km una nauli ya kurudi au lah. Anachojali ni maslahi yake tu. mathalani amefanikiwa kukuchomoa hela hata ukilala stand kwake its okey.

Namlaani sana kijana huyu na ninalaani wote wenye vitendo km hivi, vya kutumia wahitimu wa vyuo kama sehemu yao ya kuchuma kipato.

Pia natoa rai kwa vijana wenzangu wanaotafuta kazi wawe makini sana na watu wa aina hii. Usikubali kumpa mtu hela ili akutafutie/akuunganishie kazi. Kuna watu wanatumia changamoto ya ajira kwa vijana kama fursa yao ya kujipatia ajira. Walaaniwe..!!
Tag : Cate-Udaku
0 Komentar untuk "HUYU DOGO NI TAPELI BALAA...soma aliyoyafanya"

Back To Top