Flickr Photos

Gallery

MASTAA WA BRAZIL WAAMBULIA KILIO HADHARANI

Scolari



Brazil imebwagwa vibaya kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa kihistoria wa Ujerumani. Ujerumani imeitwanga Brazil mabao 7-1 yakiwa magoli mengi zaidi kuwahi kufungwa na timu moja kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia. Mvua hiyo ya magoli ilianza kwenye dakika ya 11 paleThomas Thomas Müller alipotia kimiani goli lake la tano kwenye michezo ya mara hii ya Kombe la Dunia. Baadaye yalifuata magoli 2 yaToni Kroos na 1 la Sami Khedira.

 Brazil iliyocheza bila ya nyota wake,Neymar Jr., ambaye amevunjika mgongo, ilionekana kupata uhai kwenye kipindi cha pili, lakini goli la sita na saba pia likaenda kwa Ujerumani, paleAndré Schürrle alipoongeza chumvi kwenye kidonda kibichi cha Brazil. Oscar alitia kimiani goli la pekee la Brazil katika dakika za mwisho, kikiwa ni kifuta machozi kisicholeta faraja.
Tag : SOCCER, SPORTS
0 Komentar untuk "MASTAA WA BRAZIL WAAMBULIA KILIO HADHARANI"

Back To Top