Tafiti
zinaonesha kuna idadi kubwa ya watu wanaotumia Facebook hubofya zaidi
picha au video zinazoonesha matukio yanayoendana na ngono ama picha
chafu.
Lakini imebainika kuwa baadhi ya video hizo hutumiwa na hackers kuweza kuaccess taarifa za mtumiaji na kuteka akaunti yake.
Wataalamu
wa masuala ya mitandao wa Uingereza wamewatahadharisha watumiaji wa
Facebook na kuwataka kuwa makini na video zinazosambaa zikionesha
msichana au mwanamke (hata kama wanamfahamu) akiwa anavua nguo na
kuonesha kuwa ukibofya itakupeleka Youtube kuangalia video nzima.
Wameeleza
kuwa video hizo hutuma taarifa zisizotegemewa kwenye browsers kwenda
kwenye flash player na kisha kuiba taarifa za siri za mtumiaji.
0 Komentar untuk "MATOKEO YA PICHA CHAFU FACEBOOK HAYA HAPA "