MSHAMBULIAJI
majeruhi, Neymar Jr atahudhuria mechi ya mshindi wa tatu siku ya
jumamosi kati ya nchi yake ya Brazil dhidi ya Uholanzi.
Brazil
waliomkosa Neymar katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani na
kulala kwa mabao 7-1 watachuana na kikosi cha Louis van Gaal ambao
kilitolewa jana kwa mikwaju ya penati 4-2 dhidi ya Argentina.
Neymar aliyeibeba Brazil mechi za nyuma alikosekana na kusababisha nchi yake ifanyiwe kitendo cha `Ukatili` na Wajerumani.
Nyota
huyo wa Barcelona alivunjika mfupa wa uti wa mgongo wakati wa mechi ya
nusu fainali dhidi ya Colombia nah ii ilitokana na kugongwa kwa goti
mgongoni na Juan Zuniga.
“Neymar
atakuja hapa (kwenye kikosi cha Brazil). Lengo ni kuwasapoti wachezaji
wenzake kwenye mechi ya jumamosi”. Msemaji wa Shirikisho la Brazil,
Rodrigo Paiva amethibitisha alipozungumza na R7.com.
Paiva alitangaza taarifa hizo akiwa makao makuu ya fainali za kombe la dunia, mjini Teresopolis, karibu na Rio de Janeiro.
Hata hivyo, wiki hii madaktari wa klabu ya Barcelona wameripotiwa kumtembelea mshambuliaji huyo wa Barca akiwa nyumbani kwao.
Taarifa
kutoka katika mtandao wa klabu ya Barcelona ilisomeka: “Wiki hii
Madaktari wa FC Barcelona walimtembelea Neymar Jr akiwa nyumbani kwao
nchini Brazil”.
“Viongozi wa CBF na madaktari wa Barca wapo katika makubaliano kujua aina ya matibabu atakayopata ili kuimarika kiafya”.
Kukosekana
kwa Neymar na beki aliyekuwa na adhabu, nahodha Thiago Silva
kulichangia kwa kiasi kikubwa kufungwa mabao mengi na Ujerumani ambao
watavaana na Argentina siku ya jumapili kwenye mchezo wa fainali wa
kombe la dunia.
Tag :
cate-michezo
0 Komentar untuk "NEYMAR KUUNGANA NA BRAZIL KUTAFUTA NAFASI YA 3"