Flickr Photos

Gallery

SUAREZ ATAMANI KUYANG'OA MENO YAKE KWA MKONO....click
















Shirikisho la soka duniani FIFA, limeiweka kapuni rufaa iliyowasilishwa na shirikisho la soka nchini Uruguary, iliyokuwa inapinga adhabu iliyotangazwa dhidi ya mshambuliaji wa nchi hiyo Luis Alberto Suarez Diaz mnamo June 25 mwaka huu huko nchini Brazil.
Kamati ya rufaa ya FIFA imefikia maamuzi ya kuiweka kapuni rufaa hiyo baada ya kuona hakuna sababu za kujitosheleza kufuatia utetezi uliowasilishwa mbele yao na shirikisho la soka nchini Uruguay.
Kamati hiyo pia imekiri kupokea rufaa ya mshambuliaji Luis Suarez ambayo pia ilikuwa inapinga adhabu ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa muda wa miezi minne pamoja na kutoichezea timu yake ya taifa katika michezo tisa.
Rufaa ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, pia imewekwa kapuni, kwa kukosa mashiko ya ushawishi wa kupunguziwa adhabu.
Kufuatia maamuzi hayo raisi wa shirikisho la soka nchini Uruguay, Wilmar Valdez, amesema amesikitishwa na hatua ya rufaa waliyoiwasilisha FIFA kugonga mwamba na hawana cha kufanya kwa sasa zaidi ya kuheshimu kilichoamuliwa dhidi ya Luis Suarez.
FIFA walimuadhibu Luis Suarez baada ya kujiridhisha alimg’ata kwa makususdi beki wa timu ya taifa ya Italia Giorgio Chiellini, wakati wa mchezo wa fainali za kombe la dunia kati ya The Azzuri dhidi ya Uruguay uliochezwa June 24 kwenye uwanja wa das Dunas, mjini Natal nchini Brazil
Tag : cate-michezo
0 Komentar untuk "SUAREZ ATAMANI KUYANG'OA MENO YAKE KWA MKONO....click"

Back To Top