Imechapishwa Julai 13, 2014, saa 10:14 usiku
Arjen Robben amesema kocha Louis van Gaal amemwambia kwamba kuna nafasi yake katika klabu ya Manchester United.
Winga
huyo ambaye ni miongoni mwa nyota wa kombe la dunia na alicheza mechi
ya mshindi wa tatu dhidi ya Brazil, alisisitiza kuwa ana furaha Bayern
Munich, hivyo hana nia ya kuungana na bosi wake wa timu ya taifa
anayeondoka kwenda kujiunga na Manchester United majira ya kiangazi
mwaka huu.
Aliulizwa na NOS kama
anaweza kujiunga na Manchester United majira ya kiangazi mwaka huu,
Robben alijibu: “Hapana-hata Van Gaal nimemwambia hivyo. Nina furaha
Bayern Munich,
lakini anasema kuna nafasi yangu (katika klabu ya Man United).
“Van Gaal ni moja ya makocha bora niliopitia. Tumekuwa na uhusiano wa kipekee.
“Baada
ya mechi aliniomba kujiunga na Man United, lakini sitaondoka. Nipo
sehemu sahihi Bayern Munich, kwahiyo sina lolote la kufanya na Van Gaal
au United.”.
Tangu
aondoke Chelsea mwaka 2007, winga huyo amepata mafanikio katika klabu
za Real Madrid na Bayern, akishinda taji la UEFA akiwa na klabu ya
Ujerumani mwaka 2013.
Tag :
cate-michezo
0 Komentar untuk "UNAJUA JIBU LA ARJEN ROBBEN BAADA YA VAN GAAL KUMUOMBA AJIUNGE MANCHESTER UNITED? "