Thursday, 31 July 2014 06:03
Mshike mshike wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Real Madrid dhidi ya AS Roma, uliingia katika mzimu wa mpambano wa mahasimu wakubwa nchini Hispania baada ya beki kutoka nchini Ureno Pepe kukwaruzana na kiungo kutoka nchini Mali, Seydou Keita.
Wawili hao walikwaruzana kabla ya mpambano huo wa kujiandaa na msimu haujachezwa katika mji Dallas, nchini Marekani ambapo Pepe alionekana akirushiwa chupa ya maji hali ambayo ilizua tafrani kabla ya kuamuliwa na wachezaji wenzao.
Pamoja na madhila yoye hayo Pepe alionekana ni mwenye kutabasamu na kuyapuuza yaliyotokea.
Hata hivyo kitendo hicho kilipelekea hasira kwa Keita na kujikuta akifanya maamuzi ya kutompa mkono Pepe wakati wachezaji wa AS Roma walipokuwa wakiwasalimu wachezaji wa Real Madrid kabla ya mchezo huo wa kirafiki kuanza.
Hii si mara ya kwanza kwa wachezaji hao kukwaruzana, kwani kama itakumbukwa vyema wakati wa mchezo wa Spanish Supercopa wa mwaka 2011 kati ya FC Barcelona dhidi ya Real Madrid, Keita alilumbana na Pepe baada ya kuchikizwa na maneno ya kibaguzi ambayo alidai alitamkiwa na beki huyo kutoka nchini Ureno.
_Mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya AS Roma ulichezwa usiku wa kuamkia jana, ambapo mabingwa wa barani Ulaya The Meringues walikubalia kulala bao moja kwa sifuri.
Leave a comment
Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.
0 Komentar untuk "Video: Angalia Timbwili Timbwili la Keita Vs Pepe Wakiwa Marekani"