Mgogoro
umeibuka nchini India baada ya polisi mwanamke nchini humo kucheza densi
ukumbini na muigizaji maarufu Shah Rukh Khan katika tamasha la polisi
lililofanyika katika jimbo la Bengal Magharibi.
Wanasiasa wa
upinzani wamekosoa densi hiyo, wakisema afisa huyo wa polisi kucheza
densi akiwa avelia sare zake, imehujumu heshima kwa polisi.
Polisi huyo
mwanamke na muigizaji Shah Rukh Khan bado hawajatoa tamko lolote kuhusu
sakata hiyo.Kiongozi wa jimbo la West Bengal,Mamata Banerjee,
aliyehudhuria tamasha hilo, pia alishambuliwa kwa kuruhusu tamasha hilo
kufanyika.
Densi hiyo, ilifanyika katika tamasha maalum la polisi lililofanyika siku ya Jumamosi.
Shah Rukh
Khan ni mmoja wa waigizaji mashuhuri nchini India na duniani , na hivi
maajuzi alitajwa kama balozi wa jimbo la Bengal Magharibi.
Rais wa
chama cha upinzani cha Congress katika jimbo hilo, Adhir Ranjan
Chowdhury , alituhumu mkuu wa jimbo hilo Bi Banerjee kwa kukiuka, katiba
kwa kumruhusu afisaa hiyo kucheza densi akiwa amevalia sare yake.
"katiba
hairuhusu mtu kucheza densi akiwa amevalia sare za kazi. Ni aibu tupu
kwamba sifa ya idara ya polisi ilivunjiwa heshima hivyo. Kwa kuruhusu
afisa wa polisi kucheza katika hali ile, alivunja katiba ya India, ''
alinukuliwa akisema afisa mkuu wa upinzani jimboni humo.
Taarifa
zinasema kuwa kamishna mkuu wa zamani wa polisi Nirupam Som alisema,
"wakati wa muhula wangu uongozini, singeruhusu hata kidogo polisi
kucheza densi kama vile. ''
Lakini baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii, walipuuza sakata hii iliyozua mgogoro huu wote kama kutokuwa kichekesho.
0 Komentar untuk "DANSI LAMPONZA POLISI HUYU MWANAMKE, HATARINI KUTIMULIWA KWA KUCHEZA NA SHAH RUKH KHAN "