Matatizo haya yote tutakayoelezea huchunguzwa na kutibiwa hospitali kuanzia ngazi za hospitali za wilaya, mikoa hadi rufaa.
MATATIZO KWA WANAWAKE
Kwa wanawake hukumbwa na matatizo mengi katika tendo la ndoa; kupoteza au kukosa hamu ya tendo la ndoa, hali hii hutokana na matatizo ya kisaikolojia zaidi.Mwanamke anaweza kukosa hisia kabisa za kufanya tendo la ndoa na anakuwa yupoyupo tu na kama atashiriki atakuwa aidha anaumia au anamridhisha tu mwenziye.
Hali hii inaweza kuendelea na kusababisha mwanamke akose raha wakati wa tendo, yaani hajisikii lolote na anafanya hilo tendo kwa kumridhisha mpenzi wake. Tatizo hili hutokana na mwendelezo wa tatizo la awali la kukosa hamu na chanzo kikuu kikiwa ni kutokuwepo na maandalizi ya kutosha kabla ya tendo la ndoa.Tatizo hili huwa sugu, hata ukiandaliwa vipi tatizo linakuwepo.
Maumivu wakati wa tendo la ndoa ni mojawapo ya matatizo haya. Maumivu yanaweza kuwa wakati wa tendo au baada ya tendo. Maumivu wakati wa tendo inaweza kutokana na maandalizi duni au kutokuwepo na maandalizi kabla ya tendo ambapo mwanamke anapata michubuko ukeni kutokana na uke kuwa mkavu.
Maumivu baada ya tendo hutokana na maambukizi ndani ya kizazi, baada ya tendo, mwanamke hulalamika maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.Kubana kwa misuli ya uke ni mojawapo ya matatizo haya, tatizo hili kitaalamu huitwa ‘vaginismus’. Hapa mwanamke anafanya tendo la ndoa kwa tabu kwani mwanaume anashindwa kupenya ndani na mwanamke anahisi maumivu, hata akiandaliwa vipi anakuwa tayari lakini tendo linashindikana.
Hii inatokana na mwanamke kuwa na hisia mbaya za tendo la ndoa, ni tatizo la kisaikolojia zaidi, kila akihitaji kukutana na mwenza wake uke unabana na kumpa tabu mwanaume.
Hali nyingine ambayo humletea kero mwanamke wakati wa tendo la ndoa ni kulowa sana ukeni wakati na kabla ya tendo. Hii inatokana na mambo mengi lakini zaidi ni ‘overstimulation’ yaani kuwa na hamu kubwa ya tendo la ndoa.
Hii siyo tatizo sana lakini hali hiyo ya kutokwa na majimaji mengi inaweza kudhibitiwa.
NINI KINACHANGIA?
Matatizo wakati wa tendo la ndoa huchangiwa na mambo mengi, mojawapo ni maambukizi sugu katika mfumo wa uzazi, mfano maambukizi ya fangasi, magonjwa ya zinaa, utoaji mimba au kuharibika kwa mimba hali inayosababisha upatwe na tatizo la kutokwa na majimaji au uchafu ukeni na unaweza kuambatana na muwasho au la. Matatizo katika mlango, unaweza kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa au unapojisafisha ukeni na wakati mwingine utahisi unakigusa kitu kama golori karibu na mlango wa uke kutokana na mlango wa kizazi kuvimba.
Mwanamke anaweza kupatwa na maumivu ya chini ya tumbo wakati wote au endapo atabonyeza tumbo, hii inaashiria maambukizi katika viungo vya uzazi au ‘PID’. Hali hii pia husababisha upatwe na maumivu ya kiuno yanayosambaa hadi miguuni, wakati mwingine maumivu ya kiuno husababisha tatizo la kupata haja kubwa.
Mzunguko wa hedhi unaweza kuvurugika na usijue hasa siku zako ni lini utapata yaani huna tarehe maalum, hata jinsi ya kupata au kuepuka ujauzito unakuwa huwezi kupanga.
USHAURI
Matatizo haya ya uzazi kwa wanawake huchunguzwa na kutibiwa kwa madaktari wa kinamama katika hospitali za wilaya na mkoa.
Matatizo yakiwa ya muda mrefu, huathiri mfumo wa homoni na mirija ya uzazi kusababisha ugumba.
0 Komentar untuk "MME WANGU ANANIOGOPA, HADI NIMUANZE"