Flickr Photos

Gallery

''NAMPENDA SANA WOLPER, NAOMBA TURUDIANE'' DALLAS ALILIA PENZI LA WOLPER

Sexy lady wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe.
Yule zilipendwa wa sexy lady wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe aitwaye Ramadhan Abdallah Mtoro ‘Dallas’ anadaiwa kukumbuka shuka kukiwa kumeshakucha ikielezwa kwamba eti anabembeleza kurudiana na staa huyo waliyetengana takriban mwaka mmoja uliopita ili wakamilishe taratibu za kufunga pingu za masha. 
Akizungumza na Amani  hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Lango la Jiji uliopo Magomeni, Dar, Dallas alisema kuwa anamshangaa Wolper kumkatalia ombi lake la kurudisha uhusiano wao wa kimapenzi huku akijua fika kuwa bado anampenda. “Nampenda sana Wolper. Pliz namuomba turudiane tu.

Ningejua kipindi kile nilivyorudi kutoka nje ningefunga naye ndoa kwani sasa hivi angekuwa ni mke wangu niliyechaguliwa na Mungu lakini ndiyo hataki,” alisema Dallas. Kwa upande wa Wolper alisema kuwa Dallas kwa sasa ni mshikaji wake tu na atabaki kuwa hivyo lakini kuhusiana na mapenzi, hakuna kitu kama hicho.
Ramadhan Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
“Nitasaidiana naye kwa kitu kingine lakini siyo mapenzi, kwa sasa niko na mtu wangu,” alisema Wolper. Kabla ya jahazi kwenda mrama, penzi la Wolper na Dallas lilitikisa mji huku kukiwa na maneno mengi ambayo yalimshinda mkali huyo wa filamu za Kibongo ambaye aliamua kuchukua hamsini zake.
0 Komentar untuk "''NAMPENDA SANA WOLPER, NAOMBA TURUDIANE'' DALLAS ALILIA PENZI LA WOLPER"

Back To Top