Usipomuona
mpenzi wako kwa muda moyo huingia upweke, matamanio ya kumtaka kumuona
huongezeka mara dufu, mawazo ya jinsi alivyo na kila kitu kuhusu yeye
hukufanya utabasamu na kufurahia uwepo wake kila umuonapo, na hukupa
hisia na tamaa ya
kutaka kumuona zaidi na kukufanya hitajio la kuwa naye kukuwa na hamasa zako juu yake kuongezeka na kumpenda zaidi.
Vivyo
hivyo iwapo muda mrefu ukipita bila kumuona mpenzi wako upweke huzidi
na moyo huchoka, hamasa na taamaa zinabadilika kuwa mzigo, mawazo mazuri
ya kimapenzi na husuda hubadilika kuwa msongo, njisi muda unavyozidi
kwenda na ndivyo hamasa ya mpenzi wako ndivyo inavyoisha na kuzidi
kushuka, moyo unasahau mguso wake aliokuwa nao kwako, shauku ya kuongea
inapungua, kama mlikua mnaongea kila baada ya masaa mawili kwenye simu,
masaa yatabadilika na kuwa matatu, yakiwa matatu yatabadilika kuwa siku
nzima, umbali unakuwa tena hautengenezi upweke wa kutaka kuonana bali
unawafanya mioyo yenu kusahauliana na umbali wa hisia kati yenu
kuongezeka.
Waulize
wanaume imekuandalia njia tano za kuongeza hamasa na kuondokana na
upweke unaosababisha hisia kupungua pamoja na mvunjiko wa mapenzi ndani
ya mahusiano ya mapenzi ya umbali, ukitaka mambo yako yaende salama
hakikisha unazingatia njia hizi muhimu.
- Namba 1, Hakikisha unaongea kile kilicho moyoni mwako.
Wanawake
wanauwezo mkubwa wa kugundua iwapo kuna kitu kinakusumbua na vile vile
wanawake ni rahisi sana kujihisi, kama wamekugundua
umeudhika na usipokielezea mapema akiwa amekuuliza, moja kwa moja
ataanza kujifikilia ni yeye ndio aliyesababisha au ni kwa ajiri ya
uhusiano kwa sababu yuko mbali unakuwia vigumu ila unakuwa hautaki
kuelezea wazi, kwahio kwa mahusiano ya mbali inakubidi uwe mwangalifu na
mvumilivu, kama kuna kitu kati yenu hakiendi vizuri, ni vizuri
mkakiongea kwa wakati ulio mwafaka, iwapo mkakiacha kikawajengea
kinyongo ndani ya mapenzi yenu na kufikia hatua ya kuudhiana, ugonvi wa
mapenzi kwa wapenzi walio mbali ni mgumu sana kusuruhishwa.
- Namba 2, Hakikisha mnapanga jinsi ya kukutana.
Umuhimu
wa kukutana na kuonana ana kwa ana ni mkubwa sana hasa kwa mapenzi ya
mbali, kukutana huamsha hisia na mvuto ndani ya mapenzi uliosahaulika, muda
ni dawa ya kusahau kwahio iwapo mkiacha kukutana kwa muda mrefu, yale
maumivu yanaosababishwa na upweke wa kutomuona mpenzi wako huisha na
hamasa za mapenzi pia hupungua, binadamu ameumbwa kubadilika kutokana na
mazingira, kwahio mkiruhusu muda mrefu kupita bila kuonana utofauti
lazima utaingia kati yenu hata kama mlikua na mapendo makubwa kiasi
gani, umuhimu wa kuongea hautokuwepo tena na hisia zitapolomoka na
kusababisha mvuto kuisha kabisa ndani ya uhusiano wenu.
- Namba 3, Fanyeni vitu kwa pamoja mkiwa mbali.
Kwa
tekenolojia ilivyongezeka kipindi hichi, hamuhitaji muwe mji au mtaa
mmoja ili muweze kufanya kitu cha kuwafurahisha pamoja, tafuteni kitu
kipya cha kuongelea iwe filamu au kitu chochote kingine ambacho wote
wawili mnafurahia na kupenda kukifanya au kufuatilia, mnaweza pigiana
simu na kutaalisha filamu na wote mkaanza kuiangalia kwa wakati mmoja,
pande zote mbili mnatakiwa kuwa wabunifu na mapenzi hayatawezekanika
iwapo upande mmoja pekee ukiwa unajitahidi wakati mwingine unategea na
kutokujali, na kila mkiongea hakikisha hamtumii sana neno nimekumisi,
chochote kikiwa kinatamkwa sana na kusikiwa kila siku hupoteza mvuto na
kuwa neno la kawaida na kusababisha maongezi kuisha mapema.
- Namba 4, Tambulishaneni kwa marafiki wapya na usiwe na wivu na marafiki wake wa kiume.
Kitu
kimoja uhusiano wa mbali unachosababisha ni kutoa muda mwingi wa
kutumia na marafiki, kazi yako kama mpenzi wake unatakiwa usionyeshe
wivu wako maana utakuona humuamini na kusababisha asikushilikishe kwenye
baadhi ya mambo mengine maana anajua iwapo akifanya hivyo hautohafiki
na zaidi ya hapo itasababisha ugomvi ambao haupo na itamfanya pia na
yeye kuwa na wasi wasi na wewe pia, kujiamini na kutomtilia mashaka
mpenzi wako kunatengeneza hali ya kuaminiana na kusababisha uhusiano
ujijenge katika hali nzuri ya amani na yenye msimamo zaidi.
Kutambulishana kwa marafiki wapya inawafanya muwe huru na kupata mengi ya kuongea.
- Namba 5, Ongeeni kwa kutumia njia za kuonana mara kwa mara.
Tumieni
tekenelojia iliyopo kuongeza hamasa, mvuto na chachu ndani ya mapenzi
yenu, kuonana ana kwa ana kwa kutumia njia za skype, google talk au
kutumiana video kwenye whatsaap kunaleta hali ya uhalisia zaidi na
kufanya kusimuliana kuhusu kitu cha kijinga rafiki yako alichokifanya au
mfanyakazi mwenzio anavyokuboa kuwe na hali ya mawasiliano yenye mvuto
zaidi.
Kuona
tena tabasamu lake na jinsi uso wake unapotabasamu kulipua hisia zako
maradufu na za kwake pia na kusababisha hamasa na hisia zilizosahaulika
kurejea tena kwa mara nyingine
0 Komentar untuk "SOMA MAHUSIANO YA KIMAPENZI YA UMBALI NA JINSI YA KUYAFANYA YAWE YA MAFANIKIO NA FURAHA."