Kundi la mziki wa kizazi kipya linalokuja vizuri na kushika
nafasi nzuri ya muziki wa bongofleva Tanzania Rotten Blood limeachia ngoma
nyingine inayokwenda kwa jina la FULL SHANGWE, wimbo huo ambao umeonekana kuzitesa
spika za Redionyingi hapa nchini umeachiwa huku wimbo wao wa zamani
wa Road to reality ukiwa bado unafanya vizuri katika anga ya muziki wa kizazi
kipya nchini.
Wimbo huo wa full shangwe umeonekana kupokewa vizuri na
mashabiki wa kundi hilo huku ukionekana kugeuka wimbo wa taifa kama nyimbo za akina ommy dimpo diamond nk hasa kwa baadhi ya
mashairi yake ukiwemo mstari mmoja unaoimbwa “Bia
nyagi na Madompo,Wamelewa tilalila akina Dimpoz”.
Akiongea na mtandao huu msanii wa kundi hilo Myson artist
aliweka bayana kwamba wimbo huo umewaweka
katika katika nafasi nzuri katika jamii pia wanafanya mpango wa kuiandaa video
ya wimbo huo ikiwa ni kutokana na kupokea maombi mengi kutoka kwa mashabiki wao.
“Tunafanya jitihada za kuusambaza wimbo huu na tumevifikia
vituo vingi vya radio tunashukuru mungu
kuona inapokelewa vizuri na mashabiki wetu,na kwasasa tunayafanyia kazi maombi yao ya kutaka
kuitengeneza video ya track hii”
Kundi la Rotten Blood limekuwa likifanya harakati zake za
muziki katika mikoa mbali mbali ikiwemo Dar es salaam,Dodoma,Arusha,Moshi nk na
linaundwa na wanamuziki Myson artist,Rospee,Young p na wengine wengi ambao
wanaendelea kusajiliwa ndani ya kundi hil
Tag :
BONGOFLAVA
0 Komentar untuk "KUNDI LA ROTTEN BLOOD LAMTOA JASHO OMMY DIMPOZ"