Bw.
Paulo Ndulu akijaribu kuamua ugomvi kati ya mkewe, Anitha Mapunda na
Elizabeth Chacha (mwenye shati nyekundu) anayedaiwa kuwa ni hawara yake.
KUNA matukio ambayo kama binadamu yasikie kwa
wengine tu lakini yasikutokee wewe! Kama hili la mkazi wa Ukonga
–Mzambarauni, Dar, Paulo Ndulu ambapo mkesha wa kuamkia Sikukuu ya
Sabasaba, alijikuta katika wakati mgumu pale alipoingia kibaruani kuamua
ngumi kati ya mkewe, Anitha Mapunda na Elizabeth Chacha aliyedaiwa kuwa
ni hawara yake, OFM walishuhudia.OFM ni kikosi cha kifichua maovu cha Global Publishers ambacho katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kimekuwa kikizunguka usiku ili kuhakikisha hakuna watu wanaokwenda kinyume na swaumu za Waislam.
OFM MITAANI USIKU
Siku ya tukio, majira ya saa nane usiku, OFM ilikuwa ikikatiza maeno ya Ukonga jijini Dar na kubahatika kushuhudia timbwili zito sana kutoka kwenye nyumba ya Ndulu huku majirani kibao wakiziba mtaa kushuhudia.
OFM ilisogea kwenye sekeseke hilo na kugundua kuwa, ndani ya nyumba ya Ndulu kulikuwa na kasheshe zito la nguo kuchanika kati ya wanawakwe wawili ambapo majirani walisema mmoja ni mke, mwingine hawara, kisa?
MSIKIE JIRANI
“Mke aliaga anasafiri, mume akaingiza mwanamke mwingine, sasa kumbe mke hakusafiri kikweli, alimdanganya mumewe baada ya kujua kuna mwanamke atakuja,” alisema jirani mmoja huku akilalamika kwamba, amepika daku linapoa kwa sababu ya kushuhudia filamu hiyo ya bure.
Ilidaiwa kuwa, Anitha alikuwa katika wakati mgumu baada ya mumewe kuwa na tabia ya kumwingiza mwanamke huyo ndani na kumwambia yeye akakae mahali anywe soda au aende kwao mpaka mgeni wake atakapoondoka ndipo arudi.
ALIJIFICHA
Siku ya tukio, kwa mujibu wa mashuhuda, Anitha alipobaini ujio wa mgeni huyo (Elizabeth) alijifanya anakwenda Kimanzichana, Kisarawe, Pwani lakini uhalisia alikwenda kujificha nyumba ya jirani huku akiweka wapambe wampigie chabo nyendo za mumewe kwa usiku huo kwa sababu alikuwa amechoshwa na uonevu wa kutakiwa kwenda kukaa mahali.
MUME ARUDI, HAWARA ATINGA
Chanzo kilisema saa moja usiku, Ndulu alionekana akirudi nyumbani hapo. Muda si mrefu, mrembo mweupe, mrefu alionekana akiingia nyumbani hapo na Ndulu alitoka kumpokea.
WAPAMBE WANYAKUA VIATU VYA ELIZABETHChanzo kilisema saa moja usiku, Ndulu alionekana akirudi nyumbani hapo. Muda si mrefu, mrembo mweupe, mrefu alionekana akiingia nyumbani hapo na Ndulu alitoka kumpokea.
Jirani huyo alizidi kusema kuwa, wakati Eliza akizama ndani Ndulu, alivua viatu na kuviacha nje ya mlango. Wapambe wakavichukua na kwenda kumuonesha Anitha akiwa mafichoni ili kumthibitishia kuwa tayari mumewe alikuwa na kifaa ndani.
Baada ya kuoneshwa viatu hivyo, Anitha
alichanganyikiwa na kutoka kwenda nyumbani kwake ambapo aliingia na
kusababisha varangati hilo la aina yake lililodumu kwa karibu dakika
ishirini mpaka OFM ilipotokea ambapo pia askari wa kulida doria usiku
walitinga eneo la tukio.
MJUMBE ASHIRIKISHWAIli kuweka sawa mambo ya kisheria, maafande hao wenye maadili ya kazi walikwenda hadi kwa Mjumbe wa Shina Namba 29, Mama Urio ambaye waliongozana naye mpaka kwenye eneo lenye kizaazaa.Hata hivyo, polisi na mjume huyo walimkuta Anitha ameshamvaa mbaya wake huyo huku akimtupia maneno yenye lawama na shutuma nzitonzito kwamba anamvunjia nyumba yake.
WATU DIRISHANI WEWEEE!
Ndulu mbali ya kuchoka hoi kufuatia kazi nzito na kumdhibiti mkewe asiendelee kuzichapa na Eliza, pia alikuwa na kazi nyingine ya kugombana na majirani ‘wambeya’ walijaa dirishani kwa nje wakimporomoshea maneno yenye kuudhi.
UTETEZI WA NDULU
Baada ya hali ya hewa kutulia, polisi walimuhoji Ndulu kuhusu sakata hilo, alikiri kuishi na Anitha kwa zaidi ya miaka minne lakini alimkana kuwa si mkewe kwa kuwa yeye ni Mkristo wa madhehebu ya Katoliki na hakuwahi kufunga naye ndoa.
Hata hivyo, utetezi huo wa Ndulu ulipingwa vikali na mjumbe wa nyumba kumi na polisi ambapo walimwambia kisheria mwanaume na mwanamke wakiishi ndani ya nyumba kwa muda huo tayari ni mkewe.
Wakasema kwa hiyo kitendo cha kumpelekea mwanamke mwingine ndani ni kutafuta machafuko kwa makusudi.
ELIZABETH SASA
Wakati wote wa sakata, Elizabeth alikuwa akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema amekoma kwani Ndulu alimwambia kuwa haishi na mwanamke baada ya kuachana na Anitha muda mrefu kwa sababu za ugumba.
Hatima ya sakata hilo, Elizabeth alitakiwa kurudi kwao, Ubungo -Maziwa jijini Dar na Anitha alishauriwa kwenda kulala kwa kaka yake anayeishi jirani na eneo hilo chini ya usimamizi wa mjumbe.
ANITHA MWENYEWE
Akizungumza na OFM baada ya kutulia kwa sekeseke, Anitha alisema miaka minne ya maisna na Ndulu, mapenzi yalikuwa motomoto lakini siku za karibuni mwanaume huyo alibadilika ghafla, akaamini ni baada ya kumpata Eliza.
0 Komentar untuk "FUMANIZI LA MWAKA: JAMAA AMUOKOA HAWARA WAKE ASIPIGWE NA MKEWE"