Hata hivyo, umuhimu huo haukipi kiungo hicho ukubwa wa kukizidi kichwa kwani chenyewe, achilia mbali sikio, pia kinabeba macho, pua, mdomo, ubongo, fuvu na sura! Nimeanza hivi kwa sababu staa mmoja mwenye jina kubwa sana katika muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ staili yake ya maisha inanitatiza kidogo, japo hainishangazi. Kijana huyu hana mawasiliano mazuri na baba yake mzazi, Abdul Jumaa.
Mzee huyu anamlalamikia mwanaye kwamba, licha ya kipato chake kikubwa anachokipata kupitia muziki, bado hamjali kama ambavyo mzazi anastahili. Juzikati, alipatwa na matatizo ya kuvimba mguu, lakini kijana wake akawa bize na mambo yake kiasi cha kushindwa kutoa mshiko kidogo ili baba yake apate matibabu.
Sina uhakika ni nini hasa tatizo kati yao, lakini kwa uzoefu wa maisha ya Kiswahili, unaweza kukuta kwamba kutengana kwa wazazi kumechangia. Kwamba baada ya kuachana, mama aliondoka na mtoto. Huenda, mzee hakuwajibika kwa kijana wake kama alivyotakiwa.
Haya ni matukio ya kawaida katika familia zetu. Tofauti kati ya baba na mama husababisha kuwapa matatizo watoto. Wakati mwingine akina mama hupewa mimba na wanaume kuzikataa, ukiangalia na ugumu wa maisha hivi sasa, baadhi yao huwatupa au hata kuwaua watoto wao.
Inapotokea mtoto akakua, hupewa simulizi, ama na mama au baba juu ya kilichotokea. Kuna idadi kubwa sana ya watu leo hii ambao wamekua na mzazi mmoja, wengine wakiishi kwa wajomba au hata babu na bibi zao. Katika hali halisi, inauma sana kulelewa na mzazi mmoja kwa sababu yapo baadhi ya mapenzi unayakosa kutoka kwa mzazi asiyekuwepo.
Diamond amekua akiishi na mama yake pekee. Huenda alipewa simulizi isiyopendeza kuhusu baba yake naye akaamua kuiamini. Ingawa mwenyewe amekuwa akisema kuwa aliishi katika mazingira magumu sana kabla ya kufanikiwa, binafsi simuoni kama kijana aliyetaabika kwa sababu pia amefanikiwa kimaisha akiwa na umri mdogo vilevile.
Kuishi katika mazingira magumu ni jambo moja na uhusiano na mzazi ni kitu kingine. Kuna vijana wenzake wengi tu mtaani ambao wanaishi katika mazingira magumu hadi leo, lakini wakiwa na wazazi wao wote wawili. Maana yangu hapa ni kwamba hakuna uhusiano kati ya magumu aliyopitia na kutoishi na baba yake.
Kama nilivyosema hapo juu, huenda Diamond alipewa simulizi mbaya juu ya baba yake. Najaribu kujiuliza tu, kama mzee Abdul angekuwa na mkwanja wa maana, hivi huyu jamaa asingemfuata?
Jambo moja nimshauri Diamond, wazazi wanabaki kuwa juu bila kujali matatizo yao.
Kuna watu walitupwa na mama zao, wakaokotwa na wasamaria lakini walipokua na kujitambua, waliwatafuta mama zao bila kujali simulizi walizopewa na leo wanaishi nao kwa furaha.
Fedha tunazoambiwa kwamba huyu kijana anazo, si lolote si chochote mbele ya mzazi. Unaweza kuwa bilionea wa kutupwa lakini kama huna uhusiano mzuri na wazazi wako ut aonekana huna maana mbele ya watu wenye busara zao. Kama unafikiri baba yako mzazi atakuja kukuomba msamaha kwa sababu ya pesa ulizonazo, nadhani utasubiri sana kwa vile nina uhakika hatakuja.
0 Komentar untuk "LAANA: BABAKE DIAMOND AMWANDIKIA DIAMOND MANENO MAZITO"