Keki ya msuto aliyoandaliwa Bw. Sajo.
WERAA! Watu weweee! Dume lililofahamika kwa jina
moja la Lusajo au Sajo anayefanya kazi maeneo ya Kijitonyama, Dar jirani
na duka la mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’ amejikuta akitaharuki na
kuaibika baada ya kusutwa laivu katikati ya wanawake huku akilishwa keki
na kufunguliwa mvinyo kisa umbeya, Ijumaa Wikienda limeshuhudia tukio
zima.
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la
tukio wikiendi iliyopita kabla ya gazeti hili kutua, Maimartha alidaiwa
kusuka ishu hiyo huku akiwakaribisha marafiki zake kushuhudia akiwemo
Flora Mvungi.
Ilisemekana kwamba Mai alidai kuwa kilio chake kwa muda mrefu ni
kwamba jamaa huyo amekuwa akimfuatafuata na kumwambia mumewe, Raymond
Shayo ‘Shaa’ kila jambo analolifanya dukani hapo, ikiwa ni pamoja na
kumweleza watu wa kila aina wanaoingia ndani hapo.
“Nilishapata taarifa za Sajo kuwa huwa ananichunguza, sikutaka kuwa
na haraka nikaenda naye taratibu bila kumwambia kwani nilikuwa
nikimtafutia dawa ya kumkomesha. Leo ndiyo arobaini yake imefika.“Nilishika simu ya mume wangu nikakuta SMS za Sajo zikimuomba fedha, ukweli nilichukia sana na nilishangaa kuona kumbe kazi anayoifanya ya kunichunguza analipwa, nikaona sasa ndiyo wakati wa kumkomesha kwani kwa kulipwa kwake ipo siku atatunga hata uongo kwa sababu fedha ni shetani,” alisema.
Sajo, kabla ya kujua kinachoendelea,
alikaribishwa keki na shampeini, akaenda kichwakichwa, alipomaliza
kulishwa akaambiwa asome maneno yaliyoandikwa kwenye keki ‘Sajo acha
umbeya ndoa tamu’ ndipo akachanganyikiwa na moja kwa moja msuto ukaanza
huku akiulizwa ni kwa nini anamwambia maneno mume wa Mai.
“Mh! Mimi mbona siyo kweli jamani,” alisema Sajo na kushindwa kumalizia maneno. Alipobanwa na wanahabari wetu na Gea Habibu (wa Leo Tena ya Clouds FM) juu ya kuwa na namba ya simu ya mume wa Mai, Sajo alishikwa na kigugumizi na kuondoka ambapo alikimbilia dukani kwake na kujifungia kukwepa aibu kwani siyo tukio la kawaida kwa mwanaume kusutwa kwa umbeya.
0 Komentar untuk "MAIMATHA ATENGENEZA KEKI YENYE MAANDISHI YA KUMSUTA DUME LINALOMFUATILIA"