Flickr Photos

Gallery

MKE WA KOCHA WA MAN-U AFUJISHA SIRI ZA MANCHESTER KWA WAPINZANI


Louis van Gaal na Truus wamejiunga na Manchester United kuanza ukurasa mpya wa maisha ya mpira. 
LOUIS van Gaal haogopi kukosolewa na mashabiki pamoja na vyombo vya habari, anasema mtu anayemfahamu vizuri mno kocha huyo mpya wa Manchester United. 
Mke wake Van Gaal, Truus van Gaal, ameweka wazi kuwa kocha huyo wa zamani wa Ajax, Barcelona na Bayern Munich, hawezi, hajawahi kukata tamaa pale anapokosolewa isipokuwa anaumia sana anaposhindwa kufanya kazi yake vizuri au anapomuumiza yeye. 
Watu wote wa Old Trafford watakuwa na furaha kusikia kuwa inachukua muda mrefu kumuudhi kocha huyo mwenye miaka 62-isipokuwa mke wake anayechukizwa na watu wanamuudhi mume wake. 
 Truus alisema:
Louis haogopi kukosolewa Hata kama timu yake imecheza vizuri au vibaya, hata kama watu au vyombo vya habari vitamponda au hapana, haathiriwi na kitu chochote. Mara zote ananiambia Unaogopa nini? waache wafurahie haki yao. Wewe tu ndio nakuogopa na najua mambo yalivyo kiuhalisia.
Kitu pekee kinachomuudhi ni kuona mimi naumia au nakata tamaa
Truus alikiri kuwa hafanani na mume wake kwasababu yeye anaguswa sana na matusi. 
 Siku za nyuma, nilienda kwenye mechi ya mpira wa miguu na kulikuwa na mtu mbele yangu akamtukana Van Gaal Nilimshika mabegani na kumkalipia Amekufanyia nini unamjua? mtu huyo aliogopa sana.
Kocha mpya wa Manchester United, Van Gaal, falsafa yake ni kucheza mpira wa kushambulia
Tag : M, SOCCER, SPORTS
0 Komentar untuk "MKE WA KOCHA WA MAN-U AFUJISHA SIRI ZA MANCHESTER KWA WAPINZANI"

Back To Top