kijana
ambae anahisiwa ni mwiz wa Boda boda akiwa ameuawa kwa kuchomwa na moto
na raia wenye hasira kali maeneo ya Mbagala charambe |
huu
ni muendelezo wa uchukuaji sheria mikononi kwani mapema mwaka huu
Madereva wa bodaboda walichoma Daladala kwa madai ya kugonga mtu ambapo
madereva hao walilifukuza gari hilo mpaka eneo hilo la charambe kwa
Mbiku ambapo dereva wa gari hilo alishindwa kulidhibiti akalidondosha
ndipo maderva hao wakalimwagia petroli gali hilo na kuliwasha na
kusababisha uharibifu mkubwa wa mali
lakini
uchunguzi wa blog pendwa hii unasema huyo mwananchi ambae alikua
amegongwa na hiace hiyo aliruhusiwa siku hiyo hiyo Hospitali na hakua
amepata maumivu makubwa
kutoka kwenye Meza ya paparazi
Tunawasihi
wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi kwani tabia hii imetufanya
tupoteze watu wengi bila hatia ngazi za sheria zipo kama mnamshuku ni
mwizi apelekwe kwenye vyombo vya dola ambavyo vyenyewe vitachunguza na
kujua ukweli wake na vitatoa adhabu kulingana na kosa kitendo cha kuwaua
washukiwa ni uvunjifu wa sheria na pia ww ulieuwa ndio unakua umetenda
kosa kubwa kuliko huyo mwizi uliemuua kwakua mwizi alitaka kuiba
Bodaboda wewe umeua nani mwenye kosa kubwa? wakati bado hata mioyo ya
watanzania haijapoa tukimkumbuka mwanafunzi wa Sheria Mbeya aliyeuwawa
kikatili kwa kuchomwa moto kwa kuhisiwa mwizi kumbe alienda kutafuta
chakula je hali hii ya kuwaua watu wasio na hatia itaisha lini???
Mwananchi chukua hatua waripoti watu wenye tabia hii ili umponye nduguyo
je unajuaje kesho akahisiwa,Mumeo,Mkeo,kaka yako au mdogo wako??
Tag :
Cate-Siasa
0 Komentar untuk "MWIZI WA BODABODA AUAWA KWA KUCHOMWA MOTO MBAGALA CHARAMBE "