Kama ilivyotokea kwa msanii nyota wa kike wa bongo fleva, Rehema Chalamira 'Ray C' kuingizwa katika matumizi ya dawa ya kulevya na mtu ambaye alitokea kumwamini sana, ndivyo ilivyotokea sasa kwa msanii anayefuata nyendo zake, Winfrida Josephat 'Rachel' ambapo anadaiwa kuvutishwa unga bila kujua....
Kwa
mujibu wa chanzo chetu cha karibu na msanii huyo,Rachel
amewekewa dawa hizo kupitia kwenye bangi na wakati mwingine
kwenye sigara hivyo inakuwa vigumu kubaini hila iliyofanyika....
Habari
ambazo tumezipata zinadai kwamba msanii wa kiume nyota wa
bongo fleva ambaye amewahi kutuhumiwa kutumia dawa za kulevya
ndiye anayemtengenezea kokuteli hiyo inayotarajiwa kumwangamiza
siku za usoni....
"Huyu
mtoto ameshaanza kutumia dawa za kulevya.Huwezi amini, hata Ray C
ameshapewa taarifa, hivyo anamsaka kuhakikisha anamtoa katika
kifungo alichojiingiza...
"Unajua
Ray C anampenda sana kutokana na namna anavyopenda kujiweka
kama yeye na hata jinsi anavyoimba nyimbo zake, hivyo aliposikia
madai hayo alianza kumsaka kila kona lakini bado hajafanikiwa
kwani Rachel anamkimbia," kimesema chanzo hicho.
Hata
hivyo habari zaidi zinasema kuwa kutokana na namna Rachel
anavyomuamini msanii huyo wa kiume hajakubali kama
anachanganyiwa dawa za kulevya kwenye bangi na sigara.
"Mwenyewe anajiona yupo sawa, lakini sisi tunaona tofauti, hakika Rachel anapotea na sijui nani atamuokoa.
"Tumeshamwabia
kwamba anapotea lakini haamini, tunaweza kusema kwamba Ray C
aliponea bahati, sasa sijui kama na yeye atapata bahati kama
alivyopata mwenzake, " kilisema chanzo hicho
Rachel ambaye anatamba na wimbo wa 'upepo' hakuweza kupatikana kuzungumzia tuhuma hizo
Tag :
BONGOFLAVA,
DAWA ZA KULEVYA
0 Komentar untuk "RECHAL NAYE APATWA NA MAJANGA YA UNGA KAMA RAY C"