STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans amedhihirisha
kwamba ana mahaba niue kwa mpenzi wake, Vincent Kigosi ‘Ray’ kwa
kulinadi jina lake hadharani kwa kuvaa t-shirt iliyoandikwa; ‘Ray
Kigosi’.
Staa wa filamu Bongo, Chuchu Hans akiringisha chata la msanii Mwenzake, 'Ray'.
Tukio hilo lilichukua nafasi wikiendi iliyopita kwenye Tamasha la
Usiku wa Matumaini lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar
ambapo mwanadada huyo aliambatana na mashosti zake kushuhudia burudani
tofauti ikiwemo mechi ya timu ya Bongo Fleva na Movies anayoichezea
mpenzi wake.
Chuchu Hans akipozi.
Chuchu alivaa t-shirt ya njano ambayo mgongoni ilikuwa imeandikwa Ray
Kigosi kitu ambacho hakuwahi kukifanya kabla.“Sioni tatizo kujinadi
hadharani, atakayemaindi shauri yake, nafanya kitu roho inapenda bwana
sijali maneno ya watu hata kidogo,” alifunguka Chuchu.usiku wa matumaini
2014...
0 Komentar untuk "CHUCHU ARINGISHIA PENZI LA RAY"