Jay Z na Beyonce ambao wanaendelea kupiga mkwanja kupitia ‘On The Run Tour’ iliyofanikiwa wanaripotiwa kuwa na mpango wa kutengena baada ya tour hiyo.
Kwa mujibu wa New York Post, wanandoa hao wamepanga kutengana bila kupeana talaka mara baada ya tour hiyo kwa kuwa hivi sasa wameshapokea pesa za mapromota kabla ya show na hawawezi kuahirisha kuwa pamoja.
“Wanajaribu kupanga jinsi ya kutengana bila kutalakishana. Hili tamasha kubwa na wameshapata pesa nyingi kutoka kwa mapromota ambao wamewalipa kabla.” Chanzo kililiambia New York Post.
Kimeongeza kuwa hivi sasa hawachukuliani kama wanandoa na kwamba kila mmoja ametoa pete kidoleni.
Wiki iliyopita Daily Mirror liliripoti kuwa Jay Z na Beyonce wameendelea kupata ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu kuhusu ndoa yao wakati wakiendelea tour yao.
Taarifa zinaeleza kuwa mgogoro huu unatokana na Jay Z kuendekeza tabia za michepuko huku Beyonce akiumia mara kadhaa pale anapogundua. Ugomvi unadaiwa kuanza muda mrefu lakini uliwekwa wazi zaidi baada ya Solange kumshambulia Jay Z ndani ya lift.
Vyanzo vinadai kuwa ingawa Jay Z ndiye mkosaji, anajitahidi sana kuhakikisha hawaachani huku mtoto akiwa sehemu ya sababu zinazosaidia kuwaunganisha kwa sasa.
Hivi karibuni Beyonce alidaiwa kuwatimua warembo waliongia kwenye chumba cha Jay Z cha kubadilishia nguo huku wakitolea maneno makali akiwaita mende wanaohitaji kupululiziwa dawa ya kuua wadudu.
Jay na Bey wanadaiwa kuwa na vyumba viwili tofauti vya kubadilishia nguo ingawa vinafuatana
0 Komentar untuk "MAPENZI YA JAY Z NA BEYONCE KWISHA...soma sababu"