Wasanii
wa muziki wa kizazi kipya Estelina Sanga ‘Linah’ na Nasib Abdul
‘Diamond’ wakicheza kwa pamoja katika uzinduzi wa Serengeti Fiesta 2014
jijini Mwanza.
UZINDUZI
wa Serengeti Fiesta 2014 juzikati ulirindima baada ya msanii wa kizazi
kipya anayefanya poa kwa sasa Estelina Sanga ‘Linah’, kufanya balaa
wakati wakiimba wimbo walioshirikiana na mkali Nasib Abdul ‘Diamond’
jukwaani.Wakati wawili hao wakiteka hisia za mashabiki kutokana na jinsi walivyokamua huku wakicheza shoo, pia wasanii mbalimbali nao walifanya vitu vyao jukwaani hapo, wachanga kwa wakongwe wakiwemo Young Killer na Mo music waliokuwa wenyeji.
Wakizidi kuwarusha mashabiki wao.
Wengine waliopata fursa ya kufanya makamuzi ya nguvu ni pamoja na
Yamoto Bendi, Sky Light, Makomandoo, Chege na Temba, Madee, Nay wa
Mitego, Stamina, Young Dee, Mr Blue, Nyandu Toz, Khadija Maumivu, Vanesa
Mdee na baadaye Dogo Janja aliyepanda jukwaani ikiwa ni siku chache
baada ya kutimiza umri wa miaka 18.
0 Komentar untuk "LINAH NA DIAMOND KUNA KITU KATI YENU....ona mwenyewe "